MH. BETTY MACHANGU, MBUNGE VITI MAALUMU CCM |
Serikali imetakiwa kupiga marufuku uonyeshaji wa filamu
chafu kwenye mabanda ya vichochoroni kwani zinasababisha wanafunzi wengi
kutohudhuria mashuleni na badala yake kwenda kuangalia picha hizo.
"Serikali itafanya lini opereshini ya kuwaondoa watu
wanaoonyesha picha chafu na kusababisha mahudhurio ya wanafunzi wa shule za
msingi kuwa mabaya," alihoji mbunge huyo.
Akijibu, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Juma Nkamia, alikiri kuwapo kwa uonyeshwaji wa filamu hizo katika
maeneo ya Dar es Saalam na baadhi ya miji mikubwa nchini.
Alizitaka halmashauri na Jeshi la Polisi kuchukua hatua
kuzuia vibanda ambavyo vinaonyesha picha za sinema ambazo ni chafu.
"Mara nyingi picha hizo huwa zinaonyeshwa mchana
wakijua fika kwamba wazazi wa wanafunzi wapo makazini...narudia tena kuziomba
mamlaka zinazosimamia maeneo yao kuchukua hatua za haraka," alisema.
NIPASHE
No comments:
Post a Comment