NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Bw.
Mwigulu Lameck Nchemba amejiuzulu kuanzia jana na nafasi yake kuchukuliwa na Mshauri wa
Rais Jakaya Kikwete katika masuala ya Kisiasa, Bw. Rajabu Luhwavi.
Bw. Nchemba ambaye pia ni Naibu Waziri
wa Fedha na Mbunge
wa Iramba Magharibi, alitangaza uamuzi huo Mjini Dodoma jana katika Kikao cha
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
Akizungumzia uamuzi huo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
wa CCM, Bw. Nape Nnauye, alisema Bw. Nchemba amechukua uamuzi huo ili aweze
kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Alisema awali Bw. Nchemba alimweleza Mwenyekiti wa chama
hicho, Rais Jakaya Kikwete juu ya uamuzi huo lakini rais alimshauri azungumzia
jambo hilo kwenye kikao cha NEC.
Aliongeza kuwa, jana Bw. Nchemba alilifikisha suala hilo
katika kikao hicho ambapo wajumbe wa NEC walilidhia aachie ngazi na kumtakia
mafanikio mema katika mbio za kuwania urais na kumteua Bw. Luhwavi kushika
nafasi hiyo.
MAJIRA
No comments:
Post a Comment