Kamati Kuu imepokea na kutafakari taarifa ya Kamati ya
Usalama na Maadili ambayo ilipitia adhabu waliyopewa wanachama sita waliokiuka
kanuni za Maadili na kupewa Onyo Kali, adhabu iliyodumu kwa kipindi
kisichopungua miezi 12.
Wanachama hao sita ni;-i. January Makambaii. Willium
Ngelejaiii. Steven Wasiraiv. Bernard Membev. Edward Lowassavi. Fredrick Sumaye.
Kamati Kuu imepokea na kukubali pendekezo la Kamati ya
Usalama na Maadili ya kumalizaka kwa kipindi cha adhabu kwa wanachama hawa.
Kwahiyo adhabu hiyo kwa sasa imemalizika, na wanachama hao wameruhusiwa
kuendelea na shughuli zao katika Chama.
Hata hivyo Kamati Kuu inawataka wanachama hawa na wale
wengine wenye nia ya kugombea Urais kupitia CCM Kuzisoma , Kuziheshimu na
Kuzizingatia Kanuni za Maadili za CCM na kanuni zingine zinazoongoza mchakato
ndani ya Chama, ili wasikumbwe na adhabu itokanayo na kuzivunja kanuni hizo.
Wale wote wanaotaka kugombea, yaani waliokuwa kwenye
adhabu na wengine watakaojiingiza kwenye kampeni mapema na hivyo kukiuka
maadili na miiko ya Chama, taarifa za kukiuka kwao zitatumiwa wakati wa kuchuja
majina ya wagombea utakapofika.
Taarifa hizo zitatumika katika kuwapima na kuamua iwapo
wana sifa za kutosha na wanafaa au hawafai katika kupata uteuzi wa nafasi
wanayoiomba.
Imetolewa na;-Nape Moses NnauyeKatibu wa Itikadi na
Uenezi22/05/2015
No comments:
Post a Comment