Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani wa Tanzania, akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Arusha, Bw.Onesmo Ole Nangole.
Kinyang’anyiro kwa kuwania uteuzi wa kugombea urais kwa
tiketi ya chama tawala cha CCM nchini Tanzania, kimepamba moto kwa
kwa staili ya aina yake .
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ambaye pia ni waziri mkuu
wa zamani wa Tanzania Jumamosi amejitokeza
mbele ya umati wa wanachama na
wafuasi wake katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
kuelezea kuwa ataomba uteuzi wa chama tawala kuwania urais katika uchaguzi mkuu
ambao unatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Bw. Lowassa ni miongoni mwa wanachama kadhaa wa chama tawala
ambao wameelezea nia yao ya kuomba utezi wa chama tawala ili kushiriki katika
kinyang’anyiro cha urais mwaka huu.
Baadhi ya wanachama wengine wa CCM
ambao wametangaza nia ya kutaka kuwania urais wa Tanzania ni pamoja na MBalozi
wa Umoja wa Afrika hapa nchini Marekani, Amina Salum Ali ambaye aliwahidi kuwa
waziri wa fedha wa Tanzania.
Siku chache zilizopita Balozi Amina alitangaza
kuwa anaingia katika mbio hizo za kuwania uteuzi wa chama tawala.
VOA
No comments:
Post a Comment