Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Anambra
umefungwa kufuatia viongozi wenye mamlaka nchini humo kung’amua kwamba moja ya
vyakula vinavyouzwa mgahawani humo ni nyama ya binaadamu.
Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona vichwa viwili
vya binaadamu vipya vyenye kuchuruza damu wakati walipokuwa wakiwakamata watu
kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa mgahawa huo,pia
walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya wasamaria wema kutoa
taarifa hizo za kustaajabisha!
Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya
wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye mifuko ya Rambo.
Polisi pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha
nyinginezo,seti ya magurunedi na simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa
wakiwakamata watu hao.
Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa
hasa hoteli hiyo iko karibu na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za ajabu
za watu kuingia na kutoka hotelini humo,watu wachafu na uchafu wao mwilini ni
ule usioeleweka,hivyo sikushangazwa polisi walipogundua biashara hiyo haramu
mapema wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.
Mchungaji mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya
kugundua kuwa alikuwa amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka
malalamiko yake .
Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo
asubuhi na mapema,baada ya kupata staftahi,akaambiwa kwamba pande la nyama
alilokula gharama yake ni naira 700 sawa na paundi mbili unusu alistaajabu
mno.sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya binaadamu nikaila na kwamba ilikuwa
ghali sana.
Taarifa za watu nchini Nigeria kula nyama za watu
zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu, lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua
kuuza nyama za binaadamu tu.
BBC
No comments:
Post a Comment