BAADHI ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, mkoani
Tanga, wamesema tatizo la upungufu wa walimu kwenye shule za msingi zilizopo
vijijini kunachangiwa na walimu hasa wa kike kutaka kufundisha mjini.
Walisema baadhi ya walimu wa kike wamekuwa wakighushi
vyeti vya ndoa ili
kuonesha wameolewa na kuwafuata waume zao mijini jambo
linalozorotesha jitihada za Serikali kumaliza tatizo la walimu kwani baadhi ya
shule za vijijini zina walimu hadi wawili.
"Tatizo la walimu kwenye shule za msingi linatokana
na walimu kujazana mijini hasa wa kike wakiwa na ndoa bandia, madiwani tulitenga sh. milioni 30
ili zitumike kupeleka walimu vijijini lakini sijui mchakato huo umeishia
wapi,"
Kwa upande wake,
Kaimu Ofisa Elimu wa Shule za Msingi wilayani humo, Stuart Kuziwa, alisema
tatizo la walimu ni la kitaifa likiwemo la kujazana mijini lakini hata shule
zilizopo mjini nazo zina upungufu wa walimu.
"Hata shule za mjini nazo zina upungufu wa walimu,
tumeomba kupatiwa walimu 230 kwa miaka mitatu mfululizo, hilo linaweza kumaliza
shida ya walimu katika shule za msingi," alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Amir Kiroboto,
alisema madiwani wasilalamikie tatizo la walimu kujaa mijini bali waangalie
idadi ya wanafunzi kwani shule nyingi za mjini zina wanafunzi wengi.
MAJIRA
No comments:
Post a Comment