Hivi karibuni, baada ya kuvunjika kwa urafiki wa ‘kupika
na kupakua’ kati ya mashostito wawili walio katika tasnia ya Bongo Movies, Aunt
Ezekiel Grayson na Wema Isaac Sepetu maneno hayo yametumika pasipo sababu,
Ijumaa Wikienda lina kila kitu!
Juzi, Aunt ameibuka na kutoa kauli kali bila kuuma maneno
kwamba, Wema akitangulia kuaga dunia, yeye hatakwenda kumzika kwa maana ya
kuuaga mwili wake sanjari na kuomboleza.
KISA CHA KAULI
Kauli hiyo ya Aunt imekuja siku chache baada ya Wema naye
kudaiwa kutoa kauli kama hiyo akisema kwamba, kutokana na urafiki wake na Aunt
kufa na kuwa maadui, basi hata akifa, Aunt asiende kumzika.
MSIKIE AUNT
‘LAIVU’
Ijumaa wikienda: Aunt pole kwa kulea mimba! Nina machache
sana. Wema amedaiwa kuanika hatima ya ugomvi wenu kwamba, hali ilipofikia hata
akifa wewe usiende kumzika. Wewe unasemaje?
Aunt: Kwanza nashangaa taarifa za kwamba nina ugomvi na
Wema maana hata hao ndugu zake nimesikia wanaongea mambo kibao.
“Ila mimi sioni kama kuweka picha ya tangazo la shoo ya
Zari (Zarinah Hassan) kwenye peji yangu ya Instagram ni kosa. Kwa hiyo kama
yeye hataki kuzikwa na mimi, hata mimi nasema sitamzika Wema.
AANZA KUFUNGUKA
”Halafu sidhani kama kuna mtu anaweza kunipangia kitu
kwenye peji yangu mwenyewe ambayo nina uamuzi wa kufanya chochote
ninachojisikia.
ILIKUWA UTANI,
IYOBO ATAJWA
“Mimi sidhani kama hapo kuna ugomvi, maana nilichoandika
na kuweka siku hiyo ilikuwa ni utani lakini hata kama yeye na ndugu zake
walichukulia ‘siriasi’ basi bado walitakiwa kutambua kuwa, mchumba wangu Iyobo
(Moses) ni mfanyakazi halali wa kundi la muziki la Diamond (Nasibu Abdul),
hivyo nilikuwa na haki ya kumsapoti kwa asilimia zote maana fedha anazopata
kupitia huko ndizo zinazonifanya mimi na familia yangu niishi,” alisema Aunt.
FAMILIA YAWEKA
KIKAO
Kufuatia vuguvugu hilo kushika kasi, hivi karibuni
familia ya Wema inadaiwa kuweka kikao na
kusema kwamba walimuonya ndugu yao huyo siku nyingi kwa kumwambia kuwa, urafiki
wake na Aunt ni sawa na ‘spea’ za ki-China kwani waliamini hautadumu kwa sababu
ni unafiki tu bora hata alivyokuwa na Kajala Masanja.
Chanzo makini kutoka katika familia ya Wema
kimelipenyezea ubuyu Ijumaa Wikienda ambapo kilitiririka:
“Mama Wema kama kawaida yake, alifikia hatua ya kusema
kwa sasa hataki tena kumwona mwanaye akirudia urafiki wake na Aunt kwa sababu
ni mnafiki.
MAAZIMIO YA KIKAO YAFIKA KWA WEMA
“Maneno hayo ya mama na ndugu wengine, yalifikishwa kwa
Wema, akawaelewa na kusema hana haja tena ya kuwa karibu na Aunt hata itokee
nini maana hakuna anachomsaidia.”
AUNT TENA,
AMWANIKA WEMA SASA
Aunt alipoambiwa kuhusu maazimio ya kikao cha familia ya
Wema na jinsi staa huyo alivyoyapokea, alisema:
“Kama familia yake
wamefikia hatua ya kuingilia hili, mimi nafikiri sina tatizo maana nina maisha
yangu na yeye (Wema) ana maisha yake. Ila tu kama ni ishu ya wazazi, naomba
wajue pia mimi sijajizaa wala sijazaliwa na miti, nina ndugu tena wanajitambua
kwa kila hali.
“Nikiangalia sababu za ugomvi ni za kibinafsi sana hata
hazifai kuingiliwa na mtu, maana haiwezekani kwenye maisha haya eti Wema
akinuniana na mtu basi na mimi nimnunie, sijaumbwa hivyo wala sina unafiki huo.
“Kama staili ya maisha ikiwa kila atakayekwazana naye na
mimi nimchukie siku wanapoelewana mimi si nitaonekana sifai kote? Wao wafahamu
kuwa mimi najitambua wala si wa kuburuzwa hivyo.
“Kama wanasema hawawezi kushiriki lolote kwangu hata mimi
sina sababu ya kujipendekeza kwao.
WEMA AZIDI
KUCHAMBULIWA
“Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuwa na rafiki
ambaye siku zote yeye akikosana na mtu basi na wewe ukosane naye. Mbona mimi
maadui zangu yeye ni marafiki zake na wala sijawahi kununa. Iweje sisi
tukorofishane na watu yeye aongee nao ila yeye akikorofishana na watu basi
hataki kabisa hata kutuona nao?”
WEMA NAYE ATEMA
NENO
Baada ya Ijumaa Wikienda kupata fukunyuku hizo lilimsaka
Wema kwa maana ya kujiridhisha na kinachodaiwa kusemwa na yeye na familia yake,
mambo yalikuwa hivi:
“Yaani hata sitamani kusikia jina la Aunt maana
alichokifanya ni bora hata ya Kajala ambaye ishu yake ni ya moja kwa moja.
Nashindwa kuliweka wazi sana lakini familia yangu haitaki hata kumsikia kwa
jinsi ilivyochukizwa naye.
“Sifikirii kama kuna siku nitakuja kukaa naye tena au
kuongea chochote mbele yake maana alichokifanya si cha kunifanyia mimi
tuliyeshibana kama mapacha.”
Aunt ‘mama
kijacho’ na Wema walikuwa marafiki walioshibana kabla ya kutofautiana baada ya
Aunt kutoa sapoti kwa mpenzi wa Diamond, Zari kwenye shoo yake ya Zari All
White Party kwa kuposti picha kwenye mtandao iliyoonesha kupigia debe shughuli
hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City hivi karibuni jambo lililomkera Wema
akiamini Aunt ni mnafiki, yuko kwake na
kwa mahasimu wake hao.
GPL
No comments:
Post a Comment