WANAUME nchini hapa wamepokea kwa furaha kusainiwa kwa
sheria itakayokabiliana na vitendo vya unyanyasaji hususan majumbani.
Sheria hiyo iliyosainiwa na wiki iliyopita na rais Uhuru
Kenyata, inatarajiwa kuwapa ahuweni wanaume waliokuwa wakipigwa na wake zao na
kushindwa kuripoti matukio hayo polisi.
Matukio ya wanaume nchini Kenya kupigwa na wake zao
yamezidi kuongezeka na kuhatarisha amani katika familia.
Baadhi ya wanaume walisema wamekuwa wakipigwa na wake zao
mara kwa mara na kuwafanya kutokua na amani kwenye ndoa zao.
Walisema kinga hiyo ya kisheria itakuwa ni fundisho kwa
wanawake wenye kuendekeza tabia za kuwapiga kwa kudai kuwa wameshindwa kutimiza
mahitaji ya ndoa na familia madai ambayo wameyakataa.
Kukithiri kwa matukio hayo kunasababisha kuanzishwa chama
cha kutetea haki za wanaume na kutaka kuitishwa kwa mgomo wa wanaume kwenye
ndoa mpaka sheria hiyo itakapopitishwa.
Mmoja wa waathirika wa vipigo hivyo ni Simon Kiguta,
ambaye alipigwa na kujeruhiwa vibaya na mkewe ambapo tukio hilo liliamsha
hasira za wanaume wengi nchini hapa.
UHURU ONLINE
No comments:
Post a Comment