Baada ya kipindi kirefu cha tetesi ya staa wa filamu
Wastara kuhofia maisha yake, akihisi upo mpango wa kumuangamiza kwa njia
mbalimbali ikiwepo ajali, staa huyo amesema tetesi hizo ni kweli na amekwishazitolea
ripoti polisi.
Msanii huyo amekiri kupitia eNewz kuwa, ni kweli yupo
katika tishio la maisha yake, mhusika mkubwa wa hilo akiwa mwanaume ambaye
alikuwa na mahusiano yake wa zamani ambaye hawana maelewano mazuri naye.
Wastara amesema kuwa, amekuwa na historia ya mahusiano
mabovu na mtu huyo na kupelekea kuachana naye, na kitendo cha yeye kuolewa na
marehemu Sajuki kikiwa sababu ya kuamsha ugomvi upya, na hapa anaeleza mwenyewe
mambo yalivyoanza na kujikuta katika hali hiyo na vilevile hatua alizochukua, Wastara.
Wastara amesema kuwa, mwanaume huyo amekwishamtamkia wazi
kuwa anahusika na moja ya ajali iliyomkumba, akitumia mambo ambayo ameyaita ya
kiswahili kutaka kumuangamiza, jambo ambalo amekwishalitolea ripoti polisi
takriban miaka 5 iliyopita.
Staa huyo amesema kuwa, chochote ambacho kitampata kwa
mujibu wa maelezo aliyotoa kwa mwanausalama kutokana na vitisho vya bwana huyo,
moja kwa moja vitakuwa vimemuweka hatiani, akisisitiza kuwa ana imani kuwa
maisha yake yanasonga kwa mipango ya Mungu ambayo mwanadamu hawezi kuvuruga.
EATV
No comments:
Post a Comment