POLISI mkoani Katavi imewakamata raia wapya watatu
waliokuwa wakimbizi kutoka Burundi kwa kujihusisha na biashara haramu ya meno
ya tembo.
Watu hao walikamatwa na nyara za Serikali
zenye thamani
ya zaidi ya Sh milioni 1.2.
Nyara hizo za Serikali ni vipande vitatu vya meno ya
tembo vikiwa sawa na jino moja la mnyama huyo vikiwa tayari kusafirishwa kwenda
mjini Tabora.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari
amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Frank Hamis (18) , Steven Jonas (22)
na Jackson Erasto ambao karibuni wamepewa uraia wa Tanzania.
Kidavashari alibainisha kuwa watuhumiwa hao walikutwa
juzi saa 3:00 asubuhi katika chumba alichopanga mwanafunzi wa kidato cha Nne
katika shule ya sekondari Katumba, Ernest John (19) katika eneo la Mnyasi
kijijini Katumba wilayani Mlele.
“Mwanafunzi huyo ana uhusiano nao wa kindugu hivyo
aliwakaribisha kulala chumbani kwake alimokuwa amepanga katika nyumba ambayo ni
mali ya Felix Gado iliyopo eneo la Mnyasi kijijini Katumba.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment