MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Maombezi GRC, Lusekelo
Antony ‘Mzee wa Upako’ amekiri kushirikiana na waganga wa kienyeji kujipatia
pesa kwa njia ya utapeli wakati akifanya biashara ya madini ya rubi.
Akizungumza katika ibada maalum hivi
karibuni kanisani
kwake Ubungo Kibangu jijini Dar, Lusekelo alisema utapeli huo aliufanya sehemu
mbalimbali ikiwemo mkoani Dodoma kwa kuhusisha sangoma hao ambapo walikuwa
wakimtaka mteja kuwapatia pesa huku wakimuelekeza mahali madini hayo yanapopatikana.
Alisema baada ya zoezi la kumuelekeza mteja, wao
(Lusekelo na wenzake) walitengeneza kitu kinachofanana na madini hayo ambapo
mteja hutoa pesa nyingi akiamini kuwa ni madini halisi.Kuhusu waganga hao,
alisema walikuwa wakiwaandaa feki ambapo walimchukua mteja aliyehitaji madini
hayo na kumtoza pesa nyingi ili mganga awaelekeze mahali yalipo na baada ya
hapo huchukua yale madini feki kwa wingi na kwenda kuyaficha mahali ambapo
mganga alimuelekeza mteja.
Alisema utapeli wa biashara ya madini ulimfikisha nchi
mbalimbali duniani lakini Neno la Mungu lilipomfuata aliungama na kuanza
kumtumikia yeye (Mungu).“Ulikuwa ni utapeli wa kiwango cha juu sana, kabla ya
kufikia mafanikio maishani, watu hujikuta tukipitia njia zisizo halali.
Msidanganywe na mtu yeyote, mafanikio ya kweli yanakuja kwa njia halali hadi
sasa kila nikikumbuka huwa nasema Mungu anisaidie sana,” alisema Lusekelo.
Baada ya ibada hiyo, baadhi ya waumini walisikika
wakiguna huku wakishangaa kusikia simulizi ya utapeli ya mchungaji wao.“Mmh,
kumbe mtumishi amekutana na mapito mengi sana, hadi utapeli?” walisikika baadhi
ya waumini wakati wakitoka kanisani hapo.
GPL
No comments:
Post a Comment