Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70 aliyemchoma mkewe
mwenye umri wa miaka 16 mjini Mandera kazkazini mashariki mwa Kenya amekamatwa.
Mke huyo aliyelazimishwa kuingia katika ndoa mwaka 2014
amelazwa katika hospitali kuu ya Mandera akiwa na majeraha mabaya ya kifuani
pamoja na mikononi, kiongozi mmoja wa wanawake Ubah Gedi amethibitisha.
Mwanamke huyo sasa tayari amesafirishwa hadi jijini
Nairobi kwa matibabu zaidi.
Ufichuaji huo uliofanywa kuhusu shambulizi hilo ni wa
kushangaza kwa kuwa maswala mengi ya kijinsia Kazkazini mwa Kenya yameendelea
bila kuripotiwa.
BBC
No comments:
Post a Comment