Adebayor na mama yake mzazi |
Miezi michache tu baada ya kumlaumu mamake mzazi kwa
kumroga na kumfanya apoteze fomu yake, Emmanuel Adebayor anayeichezea timu ya
Tottenham inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza, amejitokeza na
kufichua jinsi familia yake ilivyomfanya afilisike bila shukrani.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Adebayor ameeleza kuwa
"Nimekuwa nikiziweka taarifa hizi kwa muda mrefu
lakini leo nimehisi kuwa ni muhimu kuwaeleza nanyi pia. Ni ukweli kuwa masuala
ya familia hayastahili kuwekwa hadharani lakini nafanya hivi ili familia
nyingine nazo zipate funzo kupitia yaliyonisibu.
Aliandika anasema wakati alipokuwa na umri wa miaka 17, aliutumia
mshahara wake wa kwanza kuijengea familia yake nyumba.Kama mnavyojua nilipokea
tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka mwaka 2008.Nilimpandisha mama yangu
jukwaani kumshukuru yeye kwa mambo yote. Mwaka ule ule nilimleta London kwa
ajili uchunguzi wa afya yake.
Wakati binti yangu alipozaliwa niliwasiliana na mama
yangu kumweleza lakini alikata simu na sikujua ni kwanini.Soma maoni yangu ya
hivi karibuni watu wanasema mimi na familia yangu twende tupate ushauri kwa
mhubiri maarufu wa dini ya kikristo T.B Joshua.
Mwaka 2013 nilimpa mama yangu
pesa ili aende kupata ushauri kwa mhubiri huyo nchini Nigeria.
Alipaswa kukaa huko kwa wiki moja, lakini siku mbili tu
alipofika nilipokea simu kwamba ameondoka.
Zaidi ya hayo nilimpa mama yangu
pesa nyingi kuanzisha biashara ya kupika pamoja na bidhaa nyingine. Kiuhalisia
niliwaruhusu kuweka jina langu na picha yangu kwenye biashara hiyo hiyo ili
waweze kuvutia wateja.
Ni kitu gani kingine mtoto wa kiume anaweza kufanya ndani
ya uwezo wake kusaidia familia yake?
Miaka kadhaa iliyopita, nilinunua nyumba huko East Lagon
nchini Ghana kwa dola milioni 1.2 za kimarekani. Nikaona ni sawa dada yangu
mkubwa Yabo Adebayor kuishi katika nyumba hiyo. Vile vile nilimruhusu kaka
yangu Daniel naye aishi kwenye nyumba hiyo.
Miezi michache baadae nilifukuzwa kwenye nyumba
niliyokuwa naishi ikinibidi nihamie kwenye hiyo nyumba yangu. Kilichonishangaza
niliona magari mengi kwenye barabara. Kwa kweli dada yangu aliamua kuikodisha
hiyo nyumba pasipo kunieleza. Alimfukuza Daniel kwenye hiyo nyumba.
Mfahamu kwamba nyumba hiyo ina vyumba 15. Nilipompigia
dada yangu anipe ufafanuzi alichukua karibu nusu saa kunishambulia na
kunitukana kwenye simu. Nilimpigia mama yangu anielezee kisa kizima naye
akafanya kama dada yangu alivyofanya. Hivyo ni kama dada yangu alivyosema sina
shukrani.
Kaka yangu Kola Adebayor, anaishi nchini Ujerumani kwa
miaka ishirini na mitano sasa,safari zake zote za kurejea nyumbani mara nne
ametumia gharama zangu,kama hiyo haitoshi ninawasomesha watoto wake na
kuwalipia gharama zote kuhusiana na elimu yao.
Nilipokuwa nchini Monaco ,alinifuata na kutaka pesa za
kuanzishia biashra yake .Mungu pekee ndiye ajuaye nilimpa kiasi gani cha
kufungulia biashara yake,kama ukimuuliza biashara hiyo iko wapi leo?
Masahibu hayakuishia hapo,kaka yetu Peter alipoaga dunia
nilimtumia Kola kiasi kikubwa cha pesa ili arejee nyumbani,cha kushangaza
hakutokea msibani ama siku ya maziko na leo kaka yule yule (Kola) anawaambia
watu kuwa chanzo cha kifo cha kaka yetu Peter ni mimi,linawezekanaje hili?
Kaka
huyu huyu alikwenda kwenye gazeti la"The Sun" na kueleza habari za
uongo kuhusiana na familia yetu ili kujipatia fedha.
Wakatuma barua pia katika klabu ya mpira ya Madrid
nikafukuzwa.
Nilipokuwa nchini humo pia nilipata wazo kuwa ni vyema kuwa na familia
ya wana soka,hivyo nikahakikisha kaka yangu Rotimi anajiunga na chuo cha
mafunzo ya mpira huko Ufaransa. Miezi michache tu,wachezaji ishirini na saba wa
chuo hiyo aliwaibia simu za mkononi wachezaji ishirini na mmoja .Sikuongea
chochote kuhusiana na kaka Peter Adebayor ,kwasababu hayuko nasi leo hii,Mungu
ailaze mahala pema peponi ,amina.
Dada yangu sasa, Lucia Adebayor amekuwa na tabia ya
kuwaambia watu kuwa baba yetu amenitaka nimchukue dada huyu na kumpeleka
ulaya,lakini sababu kubwa hasa ni nini ya kumpeleka huko ulaya? Kila aliyeko
hapa yupo kwa sababu.
Nilirejea nyumbani Ghana nilipata taarifa za kaka yangu
anaumwa sana,niliendesha gari kwa kasi sana kuelekea Togo ili kukutana naye na
kumpa msaada anaostahili,nilipowasili huko mama yangu akanikatalia kumwona na
kunieleza kuwa ninachopaswa kufanya ni kumpa mama yangu pesa na yeye atamaliza
kila kitu.
Mungu pekee ndiye ajuaye siku ile ile nikampatia mama
yangu kiasi cha pesa alichokitaka,lakini cha ajabu watu wanalalama kuwa
sikufanya lolote kuokoa maisha ya kaka yangu Peter.
Je mimi ni mpumbavu kiasi
gani niendeshe gari mpaka Togo bure bila ya sababu?
Nikaandaa mkutano wa kifamilia mwaka 2005 ili tumalize
tofauti zetu na matatizo yanayotuzunguuka.
Nilipowauliza maoni yao wakanitaka
kuwajengea nyumba kila mmoja wao na mishahara mikubwa kila mwezi kwa kila mmoja
wao.
Leo hii niko hai wamejimilikisha kila kilicho changu je
nikifa itakuwaje?kwa sababu zote hizi,itanichukua muda mrefu mno kuweka
mikakati na misingi yangu barani Africa.kila wakati ninajitahidi kuwasaidia
wahitaji,familia yangu wao huhoji kila nifanyacho na wote huona nimefanya
uamuzi mbaya.
Ikiwa leo ninaandika haya,sina lengo la kuwaanika watu wa
familia yangu.ninataka familia zingine za kiafrika kujifunza kutokana na
ninayoyapitia mimi. Asanteni sana.
BBC
No comments:
Post a Comment