CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU),
wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, kimeendelea kuitikisa halmashauri ya wilaya
hiyo kikimtuhumu mkurugenzi wake kutoa zawadi ya bahasha tupu kwa watumishi
wake 16 bora wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani, Mei Mosi.
Taarifa ya Talgwu ambayo pia imethibitishwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ubald Wampembe, jeshi la Polisi limeanza
kuchunguza tuhuma hiyo ya matumizi ya zaidi ya Sh milioni 40 yaliyofanywa kwa
maofisa hao.
Akizungumza na wanahabari jana, Mwenyekiti wa Talgwu wa
wilaya hiyo, Andrea Mwandimbile alisema katika maadhimisho hayo yaliyofanyika
Ilula, wilayani humo, wafanyakazi hao walikuwa wapate zawadi ya kati ya Sh
250,000 na Sh 200,000 kwa kuwa watendaji bora katika kipindi cha mwaka mmoja
uliopita.Lakini walipewa bahasha tupu.
Akijibu malalamiko hayo, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema;
“kulikuwepo na tatizo dogo la mawasiliano lililochelewesha mchakato wa utoaji
wa fedha kwa ajili ya kuwapa zawadi watumishi hao.”
Wampembe alisema mchakato wa kupata fedha hizo unaendelea
kufanywa na wakati wowote kuanzia sasa watumishi hao watapewa haki yao.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment