KAMATI ya Ukweli na Maridhiano ya Chama cha Tanzania
Labour (TLP), imetangaza kumvua uanachama Mwenyekiti wa chama hicho, Agustino
Mrema.
Akizungumza jana, jijini Dar es Salaam na MTANZANIA
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joram Kinanda alisema kuwa kamati hiyo imefikia
uamuzi huo baada ya kupitia kwa kina malalamiko yaliyokuwa yakimuhusu Mrema,
ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa mbali na Mrema wengine
waliovuliwa uanachama ni Hamisi Mkadamu, Antoni Mapunda, Nancy Mrikaria,
Dominata Rwechungura, Maxmilian Lymo, Richad Lyimo, Hamisi Mkumba na Stanley
Temba.
Kinanda alisema kuwa wanachama hao wamevuliwa uanachama
kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, toleo la 2005 Ibara ya 9.9 (c) na 2009
ibara 9.5(c).
Kinanda alisema kuwa maazimio hayo yamepelekwa katika
ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa taratibu za kisheria pamoja na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa
nchini, Sisty Nyahoza, alipotafutwa ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema
kamati hiyo haitambuliki kisheria.
“Kamati hiyo haitambuliki kisheria, na hata Mrema
mwenyewe amekuwa akipinga TLP kuwa na kamati ya aina hiyo na hata viongozi wake
hawatambuliki, ” alisema
No comments:
Post a Comment