Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael `Lulu’ amekanusha
uvumi kuwa matatizo yanayowatokea wanaume aliowahi kuwa nao yanatokana na yeye
kuwa na Jini Mauti anayesababisha hali hiyo kutokea.
“Ninasali sana kwa sasa aisee, mara nyingi nafanya hivyo
mara tatu kwa siku, ninao uwezo wa kukemea mapepo na yakaondoka, hayawezi kukaa
mwilini mwangu,” alisema muigizaji huyo ambaye miaka michache iliyopita,
aliondokewa na mpenzi wake, Steven Kanumba aliyeanguka na kufariki mbele yake.
Mtabiri mmoja maarufu jijini Dar es Salaam, Maalim Hassan
Yahya Hussein, alisema tatizo kubwa linalomsumbua binti huyo ni jini mauti
ambalo baada ya kumpenda, halitaki kuridhia uhusiano wake wa kimapenzi na
binadamu.“Hapa nimshauri tu, achukue hatua ya matibabu haraka iwezekanavyo
vinginevyo hali hiyo itaendelea, anatakiwa afanye kafara kwa kuchinja mnyama
yoyote ili aondokane na matatizo haya,” alisema.
No comments:
Post a Comment