WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) Profesa Mark
Mwandosya, amesema kitendo cha kuzushiwa kufa mara tatu na kunusurika kufa
akiwa anaumwa kimeonesha jinsi Mungu
anavyompenda na kuthamini kazi yake kwa Watanzania.
Akifafanua mambo mbalimbali aliyoulizwa kuhusiana na
kuonekana akiwa mkimya,
huku watu
mbalimbali wakimtaja kuwa miongoni mwa wanaotajwa kuwania kuteuliwa na CCM
kupokea kijiti cha urais kutoka mikononi mwa rais wa awamu ya nne,
Dkt.Jakaya Kikwete, alisema amekuwa
akitumia muda mwingi kufanya kazi
za Watanzania.
Alisema mara baada ya kupona na kuimarika akiwa amepewa
wadhifa huo wa kumsaidia Rais katika ofisi yake amekuwa akitumia muda mwingi
kufanya kazi akimsaidia rais ili
Watanzania wapate maisha bora ili kuifanya imani ya aliyemteua ipate haki yake.
"Unajua mimi niliteuliwa na Rais kwa imani kubwa
nikiwa sijaimarika vema baada ya kutoka
kuugua na hivyo baada ya kuimarika Mungu
amenisaidia kwa hakika kazi yangu
kubwa imekuwa ni kufanya kazi
kusaidia Watanzania kulingana na
jinsi nilivyopangiwa na Rais," alisema Profesa Mwandosya.
Alisema kuwa ni kiongozi wa Serikali na mwanasiasa pekee
mwenye bahati kubwa ya kuzushiwa kifo
mara tatu huku taarifa zikiwa
zimesambaa bila kujua
nani alikuwa anafanya kazi hiyo. Hata hivyo alisema amekuwa na afya njema
hadi sasa akiwa anaendelea kufanya kazi za wananchi.
"Mimi naamini kuwa pamoja na kuzushiwa kifo mara
tatu Mungu aliniponya kwa upendo wake na
kwa kutambua utumishi wangu kwa Watanzania
niliouonesha tangu nianze uwaziri
katika wizara ya Uchukuzi,Mazingira, Maji na sasa katika
ofisi ya Rais,naamini Mungu amethamini kazi
yangu," alisema.
Prof. Mwandosya ambaye ni mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki,ambaye ametangaza kutowania tena nafasi hiyo
baada ya kuchaguliwa kwa nyakati
zote bila ya kupingwa huku mwaka 2005 akifanikiwa kuingia katika mchakato wa
kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kupitia CCM," alisema imani
yake ni kuwa Watanzania watapata
kiongozi makini.
Alisema amekuwa akiulizwa mara kwa mara kuhusu ukimya
wake wa kutotaka kuzungumzia masuala ya kutangaza rasmi kuwania urais ambapo amekuwa akijibu wazi kuwa
Watanzania wasubiri wakati filimbi ipigwe na chama na ndipo atakapoweza kutoa msimamo wake kwa kufuata
taratibu za chama zilizowekwa.
Alisema kuwa kinachotakiwa kwa sasa ni kwa Wtanzania
kulinda amani na utulivu wakati huu wa
kuelekea kupata Katiba Mpya na kupata
viongozi wapya watakaoweza kuongoza
katika kipindi cha awamu ya tano tangu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ianze.
MAJIRA
No comments:
Post a Comment