Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Waliarwande Lema, amejitoa kusikiliza kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa
mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi, inayowakabili
washtakiwa 11.
Tukio hilo lilitokea juzi, baada ya washtakiwa hao 11
kumuomba Hakimu Lema ajitoe kuisikiliza kesi yao ili iweze kupangwa kwa hakimu
mwingine ambaye wao wanaona atawatendea haki.
Kutokana na ombi hilo, Hakimu Lema alijitoa na
kuiahirisha kesi hiyo ambayo upelelezi wake hadi sasa bado haujakamilika na
atatajwa tena AprilI 20, 2015, itakapopangwa mbele ya Hakimu mwingine.
Mawakili wa Serikali, Ofmad Mtenga na Diana Lukondo
walidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na waliomba ipangiwe
tarehe nyingine kwa ajili ya kuitaja.
Miongoni mwa washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni
Chibago Magozi (32), John Mayunga (56), Juma Kangungu (29), Paulo Mdonondo
(30), Mianda Mlewa (40), Zacharia Msese (33), Msungwa Matonya (30), Ahmad
Kitabu (30).
Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa mnamo Novemba 3,
mwaka 2013, walifanya kosa la mauaji kinyume cha kifungu cha 196 cha sheria na
kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Chanzo: Mtanzania
No comments:
Post a Comment