MWANAFUNZI wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Pugu
jijini Dar es Salaam, Festo Filbert (11) amekutwa chumbani kwake akiwa
amejinyonga hadi kufa kwa kutumia mkanda wa kuvalia nguo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Mary Nzuki
alisema tukio hilo lilitokea jana katika eneo la Majohe kwa Ngozoma.
Alisema sababu za kujinyonga mwanafunzi huyo bado
hazijafahamika kwani hakuacha ujumbe wowote.
“Mtoto huyu alikutwa chumbani kwake anakolala akiwa peke
yake, hakuna aliyejua sababu za kifo chake,” alisema.
Alisema maiti ya mwanafunzi huyo, imehifadhiwa Hospitali
ya Amana na polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
MTANZANIA
No comments:
Post a Comment