Monday, April 20, 2015

MCHUNGAJI ANASHIKILIWA NA POLISI NIGERIA KWA KOSA LA KUWAPA MIMBA WAUMINI WAKE 20.....AMENUKULIWA AKISEMA ALIFANYA HIVYO KWAKUWA YALIKUWA NI MAONO YA KINABII..

Mchungaji Timothy Ngwu (53) wa nchini Nigeria amewapa mimba zaidi ya waumini wake 20 kwa madai ya kwamba Roho Mtakatifu alimwabia afanye mapenzi nao.

Kiongozi huyo wa kanisa la Vineyard Trinity ambaye
hivi sasa anashikiliwa na polisi nchini humo, alifanya kitendo hicho kwa waumini wanawake ambao wameolewa na wasichana wadogo ambao hawajaolewa.

Akizungumza na gazeti la NAIJ na baadaye kunukuliwa na gazeti la Jewsnews la nchini humo, Msemaji wa Kituo cha Polisi cha Enugu ambapo Ngwu anashikilikiwa, Ebere Amaraizu alisema wamemkamata kiongozi huyo kwa kosa la unyanyasaji wa kijinsia kwa waumini wanawake.

“Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba alilazimika kufanya hivyo kwani hayo yalikuwa maono ya kinabii na alifanya hivyo kwa sababu alikuwa anatii maono aliyoonyeshwa na Mungu. Maono ambayo ni kumpa mimba mwanamke yeyote ambaye Mungu amemchagua na kumwonyesha yeye kwa njia ya Roho Mtakatifu bila ya kujali kama huyo ameolewa au la,”alisema Amaraizu.

Aliongeza: “Mwanamke akijifungua atakuwa akiishi kanisani pamoja na mtoto kwa maisha yao yote.”

Mke wa mchungaji huyo ambaye baadaye alimfukuza, Veronica Ngwu ndiye aliyeenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi baada ya kuchoshwa na tabia hiyo hasa alipofikia hatua ya kumpa mimba mtoto wa kaka yake.

Ndugu wa karibu wa mchungaji huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema walimuonya kaka yao juu ya tabia hiyo, lakini hakutaka kuwasikiliza huku akidai kuwa anatekeleza agizo la Mungu.

“Hiki kilichompata kaka yetu ni hasira kutoka kwa Mungu kwa sababu tulimuonya lakini hakutaka kutusikiliza. Amekuwa mtemi hapa kwetu, anawapa wanawake mimba hovyo hovyo kwa kutumia jina la Mungu halafu ukimuonya anasema tunamuonea wivu,”alisema.

Alilalamika kuwa, Ngwu amejimilikisha sehemu ya shamba la familia yao na kufanya kanisa lake ambalo anatumia kwa kufanyia maovu hayo kwa jina la Mungu.

“Alimfukuza mke wake ambaye amezaa naye watoto watatu halafu sasa hivi anafanya kazi ya kuzaa na kila mwanamke bila kujali kama ameolewa au hajaolewa wengine ni wasichana wadogo…angalia uwanja mzima umejaa watoto wa umri na jinsia tofauti, “alilaumu.


Ndugu huyo alisema, inashangaza kuona mtu na elimu yake anafanya vitendo kama hivyo.

No comments:

Post a Comment