Nami nilivyokuwa nakua nilisikia hivyohivyo..wewe je ulishawahi sikia?
Mwalimu mkuu wa shule moja ya kiislamu mjini Melbourne,
Australia amedaiwa kuwazuia wasichana katika shule hiyo kutoshiriki katika
maswala ya michezo kwa hofu kwamba huenda wakapoteza ubikira.
Wanafunzi wa kike katika chuo cha Al-Taqwa mjini
Truganina pia walizuiwa kucheza soka kwa kuwa majeruhi huenda yakawafanya kuwa
tasa kulingana na fairfax.
Wasimamizi wa shule hiyo kwa sasa wanachunguza madai hayo
yaliowasilishwa dhidi ya Mwalimu mkuu Omar Hallak ambaye awali alizua hisia
kali baada ya kusema kuwa wapiganaji wa Islamic state walikuwa wakiungwa mkono
na mataifa ya magharibi.
Katika barua iliondikwa na wizara na kuchapishwa na The
Age,mwalimu mmoja wa zamani alisema kuwa:''Anaamini kwamba iwapo wasichana
wataruhusiwa kukimbia huenda wakapoteza ubikra wao.
Mwalimu huyo pia ana
ushahidi wa kisayansi unaosema kuwa iwapo wasichana watajijeruhi,kupitia
kuvunjika mguu wakati wanapocheza soka huenda ikawafanya kuwa tasa''..
Mwalimu huyo amedai kwamba Bwana Hallak aliwazuia
wanafunzi wa kike kutoshiriki katika mashindano ya wilaya ya mbio za marathon
mwaka wa 2013 na 2014.
BBC
No comments:
Post a Comment