MWIGIZAJI wa filamu nchini, Mariam Jolwa ‘Jini Kabula’
amesema kuwa anguko la soko la filamu za Bongo asitafutwe mchawi, kwani wasanii
wengi wanaigiza chini ya kiwango na ndiyo maana kazi zao hazifanyi vizuri,
licha ya kutumia gharama kubwa kuziandaa.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Jini Kabula
alisema kuwa ni filamu chache zinazofanya vizuri sokoni, ikiwemo ya Chozi la
Wanjaa iliyochezwa na Aunt Ezekiel, Kulwa Kikumbi ‘Dude’ na wasanii wengine
ambazo zinaonekana kuwafurahisha watu, isipokuwa nyingi zinatengenezwa kwa
kulipuliwa.
“Hakuna haja ya kumtafuta mchawi wa anguko la filamu
nchini, kwani wengi wanatengeneza kwa kulipua, endapo waandaaji wasipobadilika,
fani hii itakuwa haina maana tena kwa waigizaji,” alisema.
No comments:
Post a Comment