MWANAFUNZI wa Kidato cha Pili, Jofrey Robert
Mwakatenya (15) anatuhumiwa kuuawa kikatili na baba yake mzazi, Robert
Mwakatenya (35) baada ya kumkuta akiwa na barua ya mapenzi, inayodaiwa
aliandikiwa na rafiki wake wa kike.
Mzazi huyo ambaye ni mfanyabiashara
na mkazi wa
eneo la Majengo ‘D’ Manispaa ya Sumbawanga, anadaiwa kumwadhibu mwanafunzi
huyo, ambaye ni mtoto wake wa kwanza kwa kupiga ngumi na mateke mfululizo kwa
zaidi ya saa tatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob
Mwaruanda alithibitisha tukio hilo, lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili
iliyopita. Alisema bado wanamtafuta mtuhumiwa huyo kwani baada ya kufanya
kitendo hicho alitokomea.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,
Mwenyekiti wa Serikali Majengo D, Antony Nyambo alidai kuwa mzazi huyo alikuwa
na tabia ya kumwadhibu mwanawe huyo, akimtuhumu kuwa ni mtoro wa shule
.
“Nilitaarifiwa juu ya kisa hiki Jumapili saa
mbili asubuhi baada ya kutoka katika ibada na raia mwema, ndipo niliamua kufika
nyumbani kwa marehemu, nilimkuta akiwa amelazwa chumbani, nilipomfunua niliona
akiwa ametapakaa vumbi mwili mzima huku akiwa amevaa nguo ya ndani tu,” alidai
mwenyekiti huyo wa mtaa.
Inadaiwa kuwa usiku huo wa tukio, mtuhumiwa
alianza kumwadhibu kumpiga ngumi na mateke kuanzia saa mbili usiku hadi usiku
wa manane.
Mtoto huyo baada ya kupata kipigo hicho,
alizimia ambapo baba yake alimwagia maji mwilini hadi akazinduka, kisha
akamwamuru alale chumbani humo pamoja na mdogo wake.
Mzazi wa mtoto huyo alidamka alfajiri na kwenda
kwenye chumba walicholala watoto hao na kugundua kuwa Jofrey alikuwa
mfu.
“Ndipo baba huyo alipoaga nyumbani hapo, akidai
kuwa anaenda kutafuta gari ili Jofrey aweze kupelekwa hospitalini kwa matibabu.
Mzazi huyo hakurudi tena nyumbani kwake hadi sasa,” alibainisha.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment