Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa watoto wa kike mia
mbili na akina mama tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko
katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi hilo limesema
watoto hao waliokolewa si kati ya wale waliotekwa
mwaka mmoja uliopita na kundi
la kiislamu katika eneo la Chibok.
Jeshi limeiambia BBC kwamba
wanawake na watoto hao wa
kike walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia zimekamatwa,Msemaji
wa jeshi amesema waliwapata wasichana hao baada ya kuziharibu kambi hizo.
"Ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia
katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne
zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa kuna
wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu."
Kwa sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana
hao. Hata hivyo, jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi
waliotekwa katika mji wa Chibok.
"Tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana
ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa
umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria
wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa
Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa
zozote. "
No comments:
Post a Comment