ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima,
amesema kuna watu wanaotaka kuua kanisa lake lakini kamwe halitakufa na
litang’aa hadi katika kizazi cha mwisho.
Akizungumza katika ibada yake iliyofanyika katika Viwanja
vya Tanganyika Packers, Dar es Salaam jana, Askofu Gwajima alisema watu hao
wamekuwa wakisema kuwa hawalipendi Kanisa la Ufufuo na Uzima na kutaka life.
Alisema kanisa lake lina mamlaka na linaungana na sauti
ya damu ya mwana kondoo.
“Damu ya Yesu ina sauti kubwa ingawaje ilimwagika miaka
mingi iliyopita hivyo watu hao wanapaswa kutambua kuwa wanalindwa na Mungu kwa
njia ya damu ya Yesu.
“Hili ni kanisa la Wakristo wa Agano Jipya wasioogopa
mambo ya ajabu ajabu na ya upuuzi puuzi na anayetaka kuliangamiza kanisa hili
aangamie mwenyewe na ashindwe kwa damu ya Mwanakondoo,” alisema.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe, alitishia kuzifutia usajili taasisi mbalimbali zikiwamo za dini ambazo
alisema zinajihusisha kutoa matamko na kushawishi waumini wao kutekeleza
matakwa ya siasa.
Waziri Chikawe alisema atatumia Sheria ya Vyama vya Jamii
Sura ya 337 na kanuni zake zinazosimamia uendeshaji wa taasisi hizo.
MTANZANIA
No comments:
Post a Comment