Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Buni Ramole anayewania
Ubunge Jimbo la Moshi Mjini, juzi alitinga mkutanoni na helkopta inayomilikiwa
na Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema).
Ramole alitua na usafiri huo saa 10.37 jioni
katika
viwanja vya Pasua mjini hapa.
Hata hivyo, Ndesamburo alikiri helkopta iliyotumiwa na
Ramole ni mali yake.
Ndesamburo alisema kada huyo aliikodisha kwa dakika 30
kwa maelezo kuwa anataka kuona mandhari ya mji wa Moshi.
Kabla ya helkopta kutua eneo la mkutano, Ramole ambaye ni
mfanyabiashara, alianza kwa kuzunguka na helkopta hiyo eneo hilo.
Helkopta ilizunguka mara mbili ikipeperusha bendera ya
CCM na kutua jirani na eneo la mkutano.
Awali wakati ikiwa angani, baadhi ya viongozi wa CCM
waliokuwa jukwaani waliambia wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa helkopta
siyo upinzani kwa upinzani tu, hata wao wanayo.
Akizungumza katika mkutano huo, Ramole alisema ameilipia
helkopta hiyo kuanzia sasa hadi Oktoba.
Alisema wataitumia kufanya kampeni kutoka kata mbalimbali
hadi ushindi upatikane.
“Tutazunguka kata zote, pesa nimeshazilipa. Imetosha
sasa. Chadema wakae mbali. Safari hii tutashinda kwa kishindo na kuchukua
uongozi wa halmashauri.
“Naomba niwahakikishie nitakuwa na ninyi moja kwa moja na
mtaletewa mgombea anayekubalika na tutashinda kwa kishindo na tukishinda tuna
mpango kabambe wa maendeleoa,” alisema.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment