Wednesday, April 22, 2015

Mwanaume mmoja huko Marekani akasirishwa na kompyuta yake na kuifyatulia risasi mara 8

Mwamamme mmoja kwenye mji wa Colorado nchini Marekani huenda akachukuliwa hatua za kisheria kufuatia kisa ambapo alikasirishwa na kompyuta yake kisha akaitoa nje na kuifyatulia risasi mara nane.

Polisi wanasema kuwa Lucas Hinch alikuwa na matatizoya kiteknolojia ndipo akaipeleka kompyuta hiyo upande wa nyuma ya nyumba yake na kuiharibu ambapo alikamatwa muda mfupi baadaye.

Vyombo vya habari vilisema kuwa alichoka na kusumbuliwa na kompyuta yake lakini hakufahamu kuwa alikuwa akivunja sheria alipoiadhibu kwa risasi.

Gazeti moja lilisema kuwa wakati herufi za 
ctrl+alt+delete zilifeli , bwana Hinch alishikwa na hasira nna kuamua kulipiza kisasi kwa kuiharibu Kompyuta hiyo hadi kiwango ambacho haiwezi kutumika tena.

BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment