Taasisi ya Better Living Aid kupitia kampuni ya Royal
Nsyepa General Supplies ambayo mkurugenzi wake ni Bw Mgalula Fundikira za
jijini Dar es Salaam leo imepeleka mtaalamu wa upulizaji madawa ya kuuwa wadudu
kama kunguni na wengineo
katika kijiji cha Amani kilichopo km 6 nje ya mji wa
Tabora.
Hatua hiyo ya Better Living Aid ilifuatia ombi toka kwa wakazi wa
kijiji hicho chenye wakazi wapatao 70 ambao baadhi yao ni wazee na wenye
uathirika wa gonjwa sugu la ukoma, pamoja na changamoto ya kunguni pia wakazi
wa hao wametoa maombi kwa taasisi hiyo nawasamaria wema wengine wajengewe vyoo
zaidi kwani kwa sasa wana vyoo viwili tu vilivyo kwenye hali ya kutumika, huku
vingine vikiwa vimejaa na haviwezi kunyonyeka.
Akiongea na mtandao huu
mwenyekiti wa kijiji hicho Bw George Lusambilo alisema"kwa kweli
tunaishukuru sana taasisi hii kwa kutuletea msaada huu, kwani tumekuwa tukilala
kwa taabu sana, naona kuanzia leo tutalala kwa raha kama watu wengine" pia
aliongeza "Ila tu jamani msituchoke, bado tunakumbushia ombi la kujengewa
vyoo zaidi kwani idadi yetu na ukilinganisha na vyoo tulivyonavyo kwa kweli ni
changamoto, lakini pia tunaomba tupate hata ka zahanati kadogo ili mganga na
muuguzi wapate mahala maalum pa kutuhudumia hasa sisi wagonjwa wa ukoma"
Naye afisa ustawi wa jamii mkoa Bw Charles Makoye alisema
"kwa niaba ya serikali naishukuru sana tasisi hii ya Better Living Aid kwa
jitihada zao za kuboresha maisha ya wakazi wa hapa kijijni na napenda kuchukua
nafasi hii kutoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kusaidia kijiji hiki
kwani ustawi wa jamii si suala la serikali peke yake bali ni la jamii nzima
inayotuzunguka kwani hawa wazee wametoka huko huko katika jamii zetu.
Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid ametoa wito kwa
makampuni na watu binafsi kuiunga mkono taasisi hiyo katika jitihada zake za
kuwajengea vyoo na zahanati wakazi wa kijiji hicho.
Vile vile ameeleza dhamira
ya taasisi hiyo kutafuta wafadhili ili kujenga zahanati katika kijiji cha
Masweya, wilayani Ikungi mkoa wa Singida alisema
"Nilipata kufika kijijini
Masweya mapema mwaka huu ambako nilipata kujua kwamba wakazi wa hapo hulazimika
kutembea km 30 na ushee kwenda kjiji cha Mtunduru kupata huduma za matibabu.
Hivyo Better Living Aid itafanya kila liwezekanalo kijiji hicho kipate zahanati
japo mdogo ya kuweza kuhudumia wagonjwa wa Malaria nk pia zahanati iweze kutoa
huduma kwa wazazi, kitu mambacho kwa sasa hakipo kjijini Masweya.
Shukurani za dhati ziwaendee Mh Munde Tambwe (viti maalum
Tabora), Mh Aden Rageh (Mbunge Tabora mjini) Bibi Joha Masawe, Bi Mtagwa
Fundikira, Bibi Jamila Kaimika, Bibi Celina Koka na wanachama wote wa kundi la
Better Living Aid .
Tunashukuru kwa msaada wa hali na mali iliyowezesha kijiji
cha Amani kufanyiwa fumigation bila kumsahau mtaalamu Bw Selemani Muhogo wa
kampuni ya SILVER ENTERTRADE LIMITED aliyepulizia dawa hiyo.
ZANZIBARNEWS
No comments:
Post a Comment