Friday, April 24, 2015

Christina Shusho Anawania Tuzo za Groove Kenya

Msanii wa muziki wa injili kutoka hapa Tanzania, Christina Shusho ameingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo kubwa kabisa za muziki wa Injili Afrika Mashariki kwa mwaka 2015, Groove Awards ambazo huendeshwa huko Kenya.

Katika kipengele hicho, Shusho anachuana na wasanii wengine wakali kutoka Afrika Mashariki, Coopy Bly, Exodus, Father Micheal na Wilson Bugembe kutoka Uganda, Gaby Kamanzi wa Rwanda, na Rebecca Soki wa Congo.

Kwa sasa zoezi la kuwapigia kura washiriki kuwawezesha kushinda linaendelea kwa kipindi cha mwezi mmoja, kwa njia mbalimbali ikiwepo mtandao, kuelekea zoezi kubwa ugawaji wa tuzo hizo kwa washindi June mosi mwaka huu.

EATV

No comments:

Post a Comment