MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stephano Moshi
(SMUCCO), Mchungaji Godfrey Malisa, ametangaza nia ya kugombea urais Oktoba
mwaka huu kwa tikeki ya mgombea binafsi.
Mchungaji Malisa, alitangaza azma hiyo
huku Serikali
ikiwa bado
haijaweka bayana kuwepo kwa mgombea binafsi kwa sababu
Katiba Inayopendekezwa haijapitishwa.
Mwaka 2010, Malisa aligombea ubunge Jimbo la Moshi kwa
tiketi ya
Chama cha Tanzania Labour (TLP).
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana,
Malisa alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuamini atachaguliwa.
Alisema ameamua kuchukua uamuzi huo ili kurejesha heshima
ya
taifa, kama ilivyokuwa imejengwa na na Hayati Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Hata hivyo, alisema enzi za Mwalimu Nyerere lilikuwa na
heshima
kubwa ndani na nje ya nchi ambapo tangu kuondoka
madarakani hajaweza
kupatikana kiongozi wa kuvaa viatu vyake.
“Mimi nimeishi Marekani na China…taifa letu
lilikuwa linaheshimika, leo hii hata amani imeanza
kutoweka kutokana na maujai ya watu wenye ulemavu wa ngozi, ujambazi na wizi wa
fedha za umma,” alisema.
Katika hatua nyingine, Malisa alisema Tanzania haipaswi
kuitwa
nchi masikini kwani ina rasilimali nyingi, lakini imekosa
viongozi
wa kuzilinda na kuzitumia kuinua uchumi wa taifa.
Alipoulizwa endapo nafasi ya mgombea binafsi
haitakuwepo katika
uchaguzi huo, alisema kama Katiba iliyopo haitafanyiwa
marekebisho na
kuwapo nafasi ya mgombea binafsi, atatangaza uamuzi
mwingine.
MTANZANIA
No comments:
Post a Comment