Serikali imesema
wakati wowote kuanzia sasa itatangaza vazi la Taifa litakalowatambulisha
Watanzania mahali popote walipo duniani.
Akizungumza na
NIPASHE jana, Afisa Habari katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Concilia Niyibitanga, alisema, hadi sasa serikali imeshakamilisha
mchakato wake baada ya kupitishwa kwa mapendekezo ya sampuli mbili ya vazi la
kitenge na kanga.
Kwa mujibu wa Concilia, baada ya mchakato huo kukamilika,
kinachosubiriwa ni kwa Waziri wa wizara hiyo, Dk. Fenela Mukangara (pichani),
kulitangaza rasmi kwa umma muda wowote kuanzia sasa. Alisema, vazi hilo
lingeshatangazwa muda mrefu, lakini majukumu ya kiserikali ndiyo yaliyofanya
tangazo hilo kuchelewa kutolewa.
“Mchakato umeshakamilika, serikali imemaliza kazi yake
kwani ndiyo iliyokuwa inasubiriwa. Kuna mapendekezo ya sampuli mbili za kanga
na sampuli mbili za kitenge.
Lingeshatangazwa, lakini kutokana na Waziri kubanwa na majukumu ya
kiserikali ndiyo maana kazi imefikia hapa,” alisema na kuongeza:
“Waziri atalitangaza vazi hilo kwa umma muda wowote
kuanzia sasa. Kwa sasa anakabiliwa na majukumu ya maandalizi ya uzinduzi wa
mbio za Mwenge… baada ya kazi hiyo atatangaza, maana watu wengi wanauliulizia.
No comments:
Post a Comment