Watu kumi wamepoteza maisha katika ajali iliyotokea
katika kijiji cha ibingo kata ya Samuye mkoani shinyanga ajali iliyohusisha
basi la UNIQUE lenye namba T148BKK na LORY la kampuni ya COCA COLA lenya namba
za usajili T207BSA liliokua linakokota tela namba T655AJT.
Kwa maelezo ya abiria aliyenusurika katika ajali hiyo
Kevin Moshi ameeleza Dereva wa gari hilo alikua anaendesha kwa mwendo kasi na
walipofika katika eneo la Samuye wakakutana na Lory hilo likiwa katikati ya
barabara na ndipo ajali ikatokea.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema watu tisa
wamekufa hapo hapo na mtu mmoja amefariki wakati akipelekwa katika hospitali
lakini amewataka madereva kuendesha magari kwa kuzingatia sheria za barabara
ili kuepusha ajali ambazo zimekua zikigharimu maisha ya watu.
Naye diwani wa kata ya samuye amosi shija amesema
alishuhudia ajali hiyo baada ya kusikia kishindo kikubwa lakini basi hilo
lilikua katika mwendo mkali hali iliyosababisha ajali kutokea baada Dereva wa
basi kushindwa kupishana Lory hilo.
ITV
No comments:
Post a Comment