Taarifa zilizopo hata hivyo zinasema kwamba
hakuna raia wa Tanzania ambaye ameuawa au kujeruhiwa katika vurumai hizo ambazo
zimeanza Durban, Kwa- Zulu Natal.
Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga, amesema kwamba Ubalozi Afrika Kusini
umepeleka maofisa wake katika mji wa Durban kuangalia hali ilivyo.
Kasiga
amesema kwamba serikali imeshatoa
mwongozo wa namna ya kuwaondoa raia wake
nchini Afrika Kusini.
“Utaratibu wa kuwaondoa Watanzania upo tayari,
lakini itambulike kwamba si kila Mtanzania anayeishi Afrika Kusini ataondolewa
bali wale walio katika maeneo hatarishi.
“Tutawaondoa Watanzania ambao wanaishi katika
mazingira yaliyotishio au wale ambao mali zao zimeharibiwa,” alisema Kasiga
akizungumza na gazeti dada Daily News kwa njia ya simu jana.
Alisema kwamba Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard
Membe, ambaye yuko nje kwa safari ya kikazi atatoa taarifa mara tu
atakapowasili nchini.
“Kwa sasa waziri yupo nchini Jordan lakini
atakuwa na nafasi ya kuzungumzia suala hili mara tu atakaporejea siku chache
zijazo,” alisema Kasiga.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment