Sunday, April 26, 2015

Chama cha siasa cha ACT Tanzania kimebadili jina kwenda ACT Wazalendo

Chama kipya cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (pichani juu), kimebadili jina lake la awali la ACT-Tanzania.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini imekubali maombi
ya chama hicho huku ikiwataka kurudisha cheti cha usajili wa awali na kupewa cheti kingine.

Awali ACTL-Wazalendo ilipata usajili kwa jina la ACT-Tanzania na baadae kuomba kulibadili jina hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, ameridhika na maelezo yaliyokuwa yametolewa na uongozi wa chama hicho wa sababu za kuamua kubadili jina la chama hicho kutoka ACT-Tanzania hadi ACT-Wazalendo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari jana jiijini Dar es Salaam, Jaji Mutungu alijibu ombi hilo kwa njia ya barua.

Katika taarifa hiyo inaeleza: "Nikurejeshe kwenye barua yenye kumbukumbua namba AC-HQ/MSJ/2015 ya Aprili 15, mwaka 2015 ikisomwa sambamba na barua yangu yenye kumbukumbu namba HA.322/362/20/80 ya Aprili 13, mwaka 2015 kuhusu suala tajwa hapo juu".

Jaji Mutungi alieleza kuwa, alisoma na kuyatafakari kwa kina maelezo katika barua ya ACT-Wazalendo, na kwamba ameridhika na maelezo yao kuhusu jina jipya la chama hicho kwa mujibu wa  kanuni ya 7 ya kanuni za usajili wa vyama vya siasa.


CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment