MWANAMUZIKI Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’, ameweka wazi
kwamba yeye ni Mtanzania na si Mkikuyu kutoka Kenya kama baadhi ya mashabiki wa
muziki kutoka nchini humo wanavyomdhania.
Jay Dee ameeleza hayo baada ya kudai kwamba kila
anapokuwa katika maonyesho yake ya muziki nchini humo, mashabiki wake humtaka
ahamie nchini humo moja kwa moja.
“Unajua Wakenya wamekuwa wakisema mimi ni Mkikuyu,
wanadai natakiwa nikaishi nchini kwao wanajua mi ni Mkikuyu ila nawaeleza
ukweli ni kwamba naipenda Kenya, lakini mimi ni Mtanzania na daima nitaipenda
nchi yangu,” alifafanua Jay Dee.
Hata hivyo, katika hatua nyingine mwanadada huyo
anajiandaa kushirikiana kwa mara nyingine katika wimbo wake mpya na msanii
kutoka Burundi, Kidumu, ambaye awali walishatoa wimbo unaotambulika kwa jina la
‘Nitafanya’.
MTANZANIA
No comments:
Post a Comment