Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii iko hatarini
kutopitishwa, baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira kukataa kwa mara pili kuijadili.
Wabunge wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake,
James Lembeli,
walifikia uamuzi wa kutoijadili tena na kuwaamuru viongozi wa
Wizara hiyo wakiongozwa na Waziri Lazaro Nyalandu (pichani), kurudi tena baada
ya wiki moja wakiwa wametekeleza maagizo yaliyotolewa na kamati.
Maagizo hayo ni
pamoja na kukaidi amri ya Mahakama Kuu ya kukataa kuanza mara moja utekelezaji
wa tozo mpya kwenye Hifadhi za Taifa.
Lingine ni utaratibu wa kiingilio kwenye hifadhi na
kwamba tozo iliyotakiwa ni kila mtalii anapoingia anapoingia anatozwa kiingilio
na akitoka na kutaka kuingia tena ni lazima alipe.
Agizo lingine ni mgogoro wa mipaka kwenye Hifadhi ya
Taifa ya Saadani. Kamati iliagiza kuwa mipaka ya hifadhi hiyo ibaki kama
ilivyokuwa tangu awali, lakini kinyume chake, wizara imemega sehemu ya ardhi na
kuitafutia hati miliki.
Kutokana na maagizo hayo, Kamati hiyo juzi iliwaagiza
viongozi hao wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufika katika kamati hiyo jana
wakiwa na maelezo yote.
Licha ya maagizo hayo, viongozi wa Wizara hiyo walipofika
katika Kamati hiyo jana hawakuwa wametekeleza maagizo hayo, hivyo waliamliwa
kurudi Mei 14 mjini Dodoma wakiwa na
maelezo kamili.
Akitoa sababu za kushindwa kuwasilishwa na kutekeleza
maagizo hao, Waziri Nyarandu alieleza kuwa muda wa siku moja waliopewa na
Kamati ni mdogo kutekeleza maagizo yote.
NIPASHE
No comments:
Post a Comment