Thursday, April 9, 2015

Mtu Aliyekuwa Akikabiliwa na Kesi ya Kutangazwa Muflisi Awapiga Risasi Jaji na Wakili na Kuwaua Mahakamani huko Italy.....Haikujulikani ni kwa vipi Alifanikiwa Kuingia Mahakamani na Silaha

Jaji mmoja na wakili ni miongoni mwa watu waliouawa baada ya mshukiwa mmoja kuwafyatulia risasi ndani ya mahakama moja mjini Milan nchini Italia.

Maafisa wa idara ya mahakama wanasema kuwa mshukiwa aliyefyatua risasi ni mtu mmoja aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kutangazwa kufilisika.

Mshukiwa huyo aliwapiga risasi watu wawili ndani ya mahakama kabla ya kumshambulia jaji ambaye angelisikiliza kesi yake ndani ya ofisi yake.

Mtu wa nne anaaminika kufariki kutokana na mshtuko wa moyo.
Mshukiwa huyo alikamatwa kaskazini mwa Milan akitoroka kwa pikipiki.


Haijulikani jinsi mshukiwa huyo alivyoweza kuingia ndani ya mahakama hiyo huku akiwa na bunduki, kwa kuwa wageni wote hupitia vifaa vya kuwakagua ikiwa wana silaha.
BBC

No comments:

Post a Comment