Mkulima wa Kijiji cha Waama, wilayani Hanang’ mkoani
Manyara, Pachal Yoya amehukumiwa jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya
kufanya mapenzi na mtoto wake.
Mkulima huyo anadaiwa kufanya
unyama huo na binti huyo
(jina linahifadhi) katika nyumba ya kulala wageni.
Katika hukumu ya kesi hiyo namba 90 ya mwaka 2013, Hakimu
wa Mahakama ya Mkoa wa Manyara, Gabriel Ngaeje alisema mtuhumiwa amepatikana na
hatia dhidi ya Kifungu cha 158, Kifungu Kidogo cha 1 (b).
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Wandiba Wambura
alidai Mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 23, mwaka 2013
kwenye chumba E cha nyumba ya kulala wageni ya California iliyopo Katesh.
Wandiba alisema kuwa siku ya tukio, Yoya alitoka na
watoto wake watatu kwenye kijiji hicho na kwenda Kijiji cha Gitting kumsalimu
mjomba wao.
“Baada ya kupanga chumba, aliwanunulia chakula watoto
wake na baadaye kuwataka kulala bila nguo,” alidai Wandiba.
Alidai kuwa baada ya watoto wengine kulala, alimtaka
binti yake kuvua nguo, jambo ambalo binti huyo hakukubaliana nalo.
“Alipokataa kuvua nguo, baba yake alimvua kwa nguvu na
kumtishia kama atakataa kufanya anachotaka atamuua kama alivyofanya kwa mama
yake mwaka 2007,” alisema.
Aliendelea kudai kuwa Agosti 29, mwaka 2013 mtoto huyo
alimweleza mama yake mkubwa kuwa alibakwa na baba yake, ndipo walipokwenda
kutoa taarifa polisi na mshtakiwa kukamatwa na baadaye kufikishwa Mahakama
kujibu mashtaka ya ubakaji.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment