Staa wa Bongo Fleva, Elibarik Emmanuel ‘Nay Wa
Mitego’amefunguka uhusiano wake na mwigizaji wa filamu za Kibongo,Shamsa Ford
baada ya picha kadhaa kuzagaa mtandaoni wakiwa kimahaba wakipigana
mabusu.
Akipiga Stori na Clouds Fm alisema kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na
mwanamke yoyote kwa sasa siyo tu Shamsa Ford, na nafasi ipo kwa yoyote
anatakayekubali kuwa mpenzi wake.
‘’Jamani nipo singo kwa sasa sina uhusino na mwanamke
yoyote na Shamsa siyo mpenzi wangu,’’alisema Nay. Akizungumzia picha
zilizozagaa mtandaoni akipigana mabusu na mwigizaji huyo alisema kuwa hiyo ni
filamu yao mpya ya kimapenzi ambayo itatoka muda si mrefu kuanzia sasa.
‘’Ile picha ni vipande vya movie yetu ya kimapenzi mimi
na Shamsa bado hatujaipatia jina kwa sasa mashabiki wasubiri tu wataiona halafu
Shamsa hawezi kuwa mpenzi wangu kwa sababu ni ndugu yangu ni binamu
yangu,’’alisema Nay.
Shamsa naye alipoulizwa kuhusiano na picha hizo alisema
ni filamu yao mpya wanafanya.
No comments:
Post a Comment