MWANAMUZIKI, Judith Wambura ‘Jaydee’, anatarajia
kutambulisha wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Give me Love’ leo, katika vituo
mbalimbali vya redio hapa nchini.
Akizungumza na MTANZANIA jana, meneja wa mwanadada huyo,
Webiro Wassira ‘Wakazi’, alisema Jaydee amemshirikisha msanii na mtayarishaji
kutoka Afrika Kusini, Uhuru na Mazet.
Alisema video ya wimbo huo itaachiwa wiki ijayo,
maandalizi yake yapo katika hatua za mwisho, huku akionyesha imani yake kwamba
wimbo huo utafanya vizuri Afrika yote kutokana na ushirikiano huo.
“Jaydee ni msanii mkubwa, mipango yake ni kuhakikisha
anaendelea kulitunza jina lake kwa kufanya kazi na wasanii wengine tofauti kama
alivyofanya kwa baadhi ya wakongwe wa muziki Afrika,” alisema Wakazi.
No comments:
Post a Comment