Zile nyakati ambazo luninga ya kichogo kuwekwa juu ya meza au kabati la sebuleni zinaelekea ukingoni. Teknolojia imefanya luninga za kisasa zisikalishwe juu ya meza ili kupata muonekano angavu kutoka kila pembe. Luninga za kileo zina kipengele cha kuifunga ukutani kusaidia kuhifadhi eneo na vilevile kumwezesha mtazamaji kuona vizuri kioo cha luninga yao.
Tunapozungumzia luninga za kufunga ukutani ni aina ya plasma na LCD. Kwa siku za karibuni luninga hizi zimekuwa ni chaguo maarufu zaidi kwa wenye nyumba wengi kutokana na kuwa na muonekano angavu, pembe pana za kutazama na wigo mpana wa rangi.
Moja kati ya jambo kubwa kabisa kuhusu kufunga luninga ukutani ni sio tu nafasi unayohifadhi ukilinganisha na kama ungeweka juu ya meza au kabati au shelfu bali pia ni muonekano nadhifu kwa mapambo yako ya ndani ya ndani ya nyumba.
Unaweza ukafikiri ni kupoteza hela lakini luninga hizi za kufunga ukutani za plasma na LCD zina faida kwenye nyumba yako kwa hivyo usidharau.
Teknolojia hii mpya sio tu kwa ajili ya muonekano angavu na mfumo bora wa sauti, ni kuwa hizi luninga za kioo kilicho flati na za kufunga ukutani zinawasaidia wenye nyumba wengi kutimaza upya nafasi ya sakafu iliyokuwa ikipotea, kwenye sebule, kwenye vyumba vya familia na hata kwenye vyumba vya kulala.
Kufunga luninga ukutani inakufanya kuondokana na hilo kabati, meza ama shelfu la sebuleni na hivyo kuboresha nyumba yako kuliko hata hiyo luninga yenyewe.
Kuweza kufunga luninga ukutani unatakiwa kuwa na fundi anayejua jinsi ya “kucheza” na ukuta kwa maana ya kuutoboa, kuunganisha waya za umeme na luninga na jinsi ya kuficha mrundikano.
Kuna mambo muhimu ya kuzingatia kabla hujaamua kufunga luninga yako ukutani ambayo ni pamoja na kuamua ni ukuta upi unataka kufunga, waya zitakaa kaaje, muonekano, ukubwa na uzito wa luninga.
Nyingi ya luninga hizi za plasma na LCD ambazo zinapendeza zaidi zikifungwa ukutani zina vifaa maalum vya kufungia ambavyo unatakiwa kununua kulingana na ukubwa na uzito wa luninga yako.
Katika kuamua ni wapi pa kufunga, fikiria ni wapi unapojisikia burudani zaidi wakati unapotazama luninga, unapendelea iwe juu ya usawa wa jicho ukiwa umekaa au iwe levo sawa na macho?
Je unataka sauti kila mahali au ni eneo fulani tu la chumba. Kikawaida inatakiwa jicho lako liende katikati ya kioo cha luninga ukiwa umekaa.
Unatakiwa kukaa raha mustarehe wakati ukitazama luninga. Pia, kuna uwezekano wa kuona picha vizuri zaidi kichwa kikiwa wima kuliko kikiwa kwenye pembe.
Kaa kwenye
Fahamu kwa kina mahitaji yako ya burudani. Vyumba vya thieta za nyumbani kwa mfano, vinahitaji spika sahihi kwa sauti sahihi. Mahali pa kuweka spika napo panahusika kwa spika mbili au nne kuhitajika kuwekwa mbele ya luninga. Na nyingine mbili kwenye kona nyingine za maeneo ya kukaa.
Baadhi ya luninga ni nzito sana kufunga ukutani kwa hivyo kama nyumba yako ni ya zamani sana au haina kuta imara, utatakiwa kutanguliza mbao ngumu.
Ukubwa pia unahusika kwenye kufunga luninga ukutani kwa ajili nati maalum vya kufungia vinaweza kufanya kazi kwa luninga zenye uzito na ukubwa fulani. Haijalishi aina ya ukuta ilipofungwa, luninga inatakiwa iwe imefungwa imara kiasi cha kuzuia isianguke, na pia isicheze cheze hata
Waya zinakaaje? Baadhi ya watu wanatoboa ukuta na kudumbukiza waya upande mwingine wa chumba ili kufanya chumba cha luninga kisiwe na mrundikano wa waya. Hata hivyo wengi wanapendeleaa kuwa na kila kitu yani luninga na waya kwenye chumba kimoja na kwa maana hiyo kuna jinsi ambayo fundi anaficha waya nyuma ya luninga iliyofungwa ili zisionekane.
Walio wengi wanaweka
luninga zao za plasma au LCD juu ya stendi au meza au fenicha nyingine. Lakini
ni burudani gani iliyoko hapo? Moja ya faida ya kuwa na kuninga isiyokuwa ya
kichogo ni uwezo wa kuifunga moja kwa moja ukutani!
No comments:
Post a Comment