Thursday, April 2, 2015

KWA MWEZI WAJAWAZITO 10 WANAOLAZWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA KAGERA HUFA KWASABABU YA KUTOA MIMBA KIENYEJI

IMEELEZWA kuwa kati ya wajawazito kumi ambao hulazwa katika hospitali ya mkoa wa Kagera kwa mwezi mmoja hufa kwa sababu ya kutoa mimba kwa njia za kienyeji.
Kauli hiyo ilitolewa na mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Juma Nyakina jana wakati akizungumza na mwandishi wa habari aliyefika hospitalini hapo kwa lengo la kujua sababu kubwa za kutokea vifo vya wajawazito.

Nyakina alitoa mfano wa kipindi Julai hadi Desemba mwaka jana ambapo kati ya wajawazito wanane waliopoteza maisha hospitalini hapo watano walikufa baada ya kutolewa mimba kienyeji.

Alisema watu hao walitokwa damu nyingi ambapo walifikishwa hospitalini hapo wakiwa wameishiwa damu kabisa huku wakiwa na hali mbaya iliyosababisha wafariki kabla au wakiwa wanapatiwa huduma.


Alizitaja sababu kubwa za wajawazito kupoteza maisha katika hospitali hiyo kwa sasa kuwa ni sababu ya kwanza ni utoaji wa mimba kwa njia za kienyeji, utokwaji wa damu nyingi baada ya kujifungua, kubanduka kwa kondo la nyuma kabla ya kujifungua na Malaria.
CHANZO: HABARI LEO

No comments:

Post a Comment