Maafisa wa Kenya wanasema wamemtambua mmoja wa wavamizi
wa al-Shabab waliouwa watu 148 chuo kikuu cha Garissa April 2 kama mtoto wa
afisa wa serikali ya Kenya.
Afisa mmoja wa Garissa aliliambia shirika la habari la
Reuters kuwa serikali ilikuwa na habari kuwa Abdullahi, ambaye alikuwa
mwanafunzi wa sheria katika chuo kikuu cha Nairobi, alikuwa amejiunga na kundi
la kigaidi la al-Shabab baada ya kumaliza chuo 2013.
Waombolezaji wakiwa nje ya hospitali Nairobi kutafuta
maiti za ndugu zao
Waombolezaji wakiwa nje ya hospitali Nairobi kutafuta
maiti za ndugu zao
Wakati huo huo, makanisa nchini Kenya yalitumia walinzi
wenye bunduki kulinda waumini wao Jumapili wakati misa za Pasaka zikifanywa
maalum kuwaombea waliouawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya Alhamisi.
Kwa mamia ya wakristo Garissa misa za Jumapili zilijaa
majonzi kutokana na shambulizi hilo. Watu wenye bunduki walivamia chuo kikuu
cha Garissa Alhamisi April 2 na kufyatua risasi na kuuwa watu 148 wengi wao
wakristo, ingawa al-Shabab inajulikana pia kwa kuuwa waislamu katika siku za
nyuma.
No comments:
Post a Comment