Tuesday, April 7, 2015

Mwanaume Mwenye Wapenzi 17 China

Mwanamume mmoja raia wa Chini anaendelea kupata ahueni baada ya kupata ajali ya gari ,lakini akajikuta katika wakati mgumu baada ,wakati mabibi zake wote kumi na saba walipoamua kwenda kumjulia hali katika hospitali alikolazwa.

Shababi huyo anaitwa Yuan, anayetokea Changsha,alipatwa na ajali ya gari mwezi March 24 na amelazwa hospitalini tangu wakati huo.wanawake hao hawakuwahi kujua kuwa bwana Yuan ana idadi hiyo ya wanawake,na hakuna aliyedhani kuna aliyemzidi,mmoja wao aliishi na Yuan kwa muda wa miaka tisa na kujaaliwa mtoto mmoja wa kiume,na bado hakutanabahi kuwa wako wengine kumi na sita nyuma yake.

Mwanamke huyo aling’amua siri ya laazizi wake baada ya madaktari kuwapigia simu wanawake wote kuwataarifu kuwa bwana wao ameumia ajalini.

Bibi mmoja aitwaye Xiao Li, alikuwa akijiachia kimahaba na shababi Yuan kwa miezi kumi na nane amesema kwamba nilipatwa na mashaka makubwa baada ya kutaarifiwa mkasa uliomfika,lakini nilistaajabishwa na idadi ya warembo waliokuwa wakiingia kila dakika kumjulia hali,niliacha kulia papo hapo .

Mrembo mwingine aliropokwa kwamba haelewi ingekuwaje mbeleni,kwani alishaanza mipango ya harusi na bwana Yuan.

Wang Fang, mama mwenye mtoto wa kiume aliyezaa na Yuan,amevurugwa na hali ya bwana huyo kiasi cha kujiuliza maswali yasiyo na majibu kuwa afanye nini sasa, akajikuta akisema hampendi Yuan tena lakini anampenda mtoto wake wa kiume.

Uso wa Yuan ulikua mdogo, baada ya siri yake kubumburuka.

Wanawake hao wakaona isiwe taabu wamefungua kijikundi chao katika Facebook,kwa lengo la kufungua mdahalo wa majadiliano juu ya kisanga chao hicho,na pia kutaka kujua walivyochezewa shere na shababi huyo.

Habari hii imezusha gumzo katika mitandao ya kijamii,walio wengi wakimlaumu mwanamume huyo kwa kitendo chake na wengine walivutiwa na uwezo wake wa kucheza na wanawake kumi na saba kwa wakati mmoja.

Kutokana na hali hiyo Polisi nchini China wameanzisha uchunguzi kuhusiana na madai ya udanganyifu alioufanya bwana Yuan,na ni mapema mno kuzungumzia lolote juu ya mabibi wa bwana huyo kuwa ni waathirika wa kashfa ya kimapenzi.

BBC

No comments:

Post a Comment