WATU sita wamekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka
mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Juma
Saad Khamis, alisema hilo ni moja ya matukio mabaya kuripotiwa kufanywa katika
kipindi cha maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka.
“Watu hao walikamatwa Jumapili saa 2 usiku
wakihusishwa kuhusika na tukio hilo,” alisema.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa siku ya tukio
watuhumiwa walionekana wakinywa na mwanamke huyo na baadaye walianza kumpiga na
kumchukua hadi maeneo ya Bwejuu.
Hata hivyo Kamanda Khamis alikataa kutoa maelezo
ya kina kuhusiana na watuhumiwa hao kwa maelezo kuwa yanaweza kuvuruga
upelelezi wa tukio hilo ambao unaendelea kufanywa na mamlaka husika.
Alisema ukiacha tukio hilo baya, wananchi
walisherehekea kwa amani sikukuu ya Pasaka.
“Kulikuwa na amani, nawashukuru polisi wa doria
kwa kazi yao nzuri na kusababisha wananchi kusherehekea sikukuu kwa amani,”
alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Mkadam Khamis Mkadam.
Kamishna Msaidizi (ACP) Mkadam alisema kulikuwa
na matukio madogo ya ajali za barabarani, naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kaskazini Unguja Mohamed Msangi alisema katika mkoa wake hakukuwa na matukio
mabaya.
Chanzo Habari Leo
No comments:
Post a Comment