KUTOKA alphaigogo.com
Nafikiri wote tumesikia na kusoma kwenye
mitandao mbali mbali kuhusu ndoa ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr.
Reginald Mengi na former Bongo Flava
Artist Jacqueline Ntuyabaliwe (K-Lynn). Ndoa hiyo ambayo inasemekana kufungwa
katika visiwa vya Mauritius na watu wachache sana wameweza kuhudhuria tukio
hilo; katika hao watu wachache inasemekana hakuna mtoto wake hata mmoja
(kutoka
kwa ndoa yake na mke mkubwa) ambaye alikuwa hapo kushuhudia tukio hilo. Pia
vile vile hakuna ndugu wala jamaa wa karibu kabisa wa Dr. Mengi ambaye
alialikwa kushuhudia ndoa hiyo! Hili
swala limenikumbusha kitu ambacho kilishawahi tokea miaka ya huko nyuma ambacho
kilipelekea Mr. Mengi kuita waandishi wa habari na kukanusha tuhuma hizo.
Mwaka 2009 kuna picha zilitumwa mitandaoni ambazo
zilionyesha Dr. Mengi na mdada aitwaye Lilian Kimaro ( wengi tuliziona) pamoja
na watu wengine wakiwa kwenye sherehe fulani.
Mavazi yao na mazingira ya party yalikuwa yakiashiria watu hao wawili na
wengine walio kuwepo kwenye picha kuwa ilikuwa ni sherehe fulani muhimu.
Wajuzi
wa habari wakitoa taharifa kwamba by then Mr. Mengi now ni “Dr. Mengi” amefunga
ndoa na mrembo huyo (Lilian Kimaro), kitu ambacho Dr. Mengi alikuja akakanusha
kwa kusema ni kuwa ni uzushi tuu wakutaka kumchafulia jina, pia akahusisha
jambo hilo na jitihada zake za kupinga ufisadi. Unaweza kujikumbusha story hiyo
kwa link hizi zifuatazo:-
1)
http://issamichuzi.blogspot.com/2009/02/mengi-avunja-ukimya-juu-ya-ndoa-yake.html
2) http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/24174-moto-umewawakia-hawawezi-kuuzima-mengi-4.html
3)
http://www.bongocelebrity.com/2009/02/11/%E2%80%9Csijaoa%E2%80%9D-reginald-mengi/
Kitu ambacho kilishangaza wengi hata mimi ni kitendo cha
Dr. Mengi kukataaa kuhojiwa kuhusiana na ndoa au picha hizo. Pia watuhumiwa
walio husika katika sakata hilo Ms. Lilian Kimaro, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni by then was Lt.
Col. Fabian Massawe hawa wote hakuna aliye kuja mbele na kukanusha tuhuma hizo
mpaka leo. Sasa basi, mie nikajiuliza hivi; kama ni kweli hakuna mtoto wake
kutoka ndoa ya kwanza wala ndugu wakaribu walioudhuria, hii ndoa ya leo ya Dr.
Mengi na K-Lynn ni yakweli? au tusubiri siku Mengi ajekuita waandishi wa habari
na kukanusha tena kuwa ni uvumi tuu? SMHO!!
Street is talking kwamba ndoa ya Dr. Mengi na mkewe Mercy
is still valid (yani hawajatalikiana), kutokana na ukweli ya kwamba ndoa hiyo
ilikuwa ni ya kanisa (until death do us apart).
Sasa hapa ndipo ninapoomba msaada wa sheria katika maswali yafuatayo:-
1. Kama ni kweli ndoa ya kwanza haijatengulia, je Dr.
Mengi atakuwa amevunja sheria ya inchi kufunga ndoa na K-Lynn hata kama ndoa
imefungwa inchi nyingine?
2. Assume Dr. Mengi hakuweka wazi nani atakuwa muamuzi
wake mkuu katika maswala ya afya. Je, kama ikatokea Dr. Mengi amepata matatizo
ya kiafya na hawezi kufanya maamuzi muhimu, je inawezekana k-Lynn akawa na
final say as it seems Dr. Mengi and his first wife doesn’t get along?
3. Kwakuwa K-Lynn anawatoto na Mr. Mengi, je hao watoto
watakuwa part of Mengi’s estate hataka ndoa hiyo ikagundulika kuwa batili?
4. Kama mke mkubwa akajatambua kwamba kweli kuna ndoa
imefungwa wakati yeye bado ana ndoa halali na Dr. Mengi, je, kisheria
naruhusiwa kumfikisha Dr. mengi mahakamani na kumshitaki? Naomba mtusaidie
kujua atamshitaki kwa kutumia kipengele kipi cha sheria?
Asanteni!
No comments:
Post a Comment