Mbunge wa zamani wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mussa
Lupatu ni miongoni mwa waliofariki katika ajali ya basi kijiji cha Mbwewe,
Mkata wilayani hapa.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Juma
Ndaki, Lupatu alipata ajali hiyo akitokea Kibaha kuelekea Korogwe kumpeleka
mwanae, Idrisa Lupatu, ambaye naye ni marehemu kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa
akili.
Wengine waliyotajwa kufariki katika ajali hiyo ni karani
wa Mahakama ya Ardhi Dar es Salaam, Devota Msimbe, aliyefariki akikimbizwa
Hospitali ya Muhimbili.
Wengine waliotambuliwa ni Secilia Temba na watoto wake
wawili, Wilfred Temba na Heppnes Temba, akiwamo dereva wa basi la Ngorika, Abas
Mwamsele na Marry Serango, wakazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Aidha, Ndaki alisema maiti tatu hazijatambuliwa na miili
yao imehifadhiwa katika hospitali ya magunga wilaya Korogwe.
Aidha, majeruhi 12 kati ya 34 wamelazwa katika hospitali
tofauti, wakiwamo saba waliopelekwa Muhimbili, mmoja hospitali ya wilaya ya
Handeni na wanne kituo cha afya Mkata, wilayani Handeni.
MUHIMBILI
Waliyolazwa Muhimbili ni Suli Murutu (46) mkazi wa
Chanika, Dar es Salaam, Said Salum (35), dereva wa basi la Ratco, Mohamed
Bashiri (23), mkazi wa Dar es Salaam, Augustino Lupatu, mkazi wa Kihaba,
Mohamed Abdul na wawili waliotambuliwa kwa jina moja la Boazi na Soshi.
HANDENI
Majeruhi waliolazwa katika hospitali ya wilaya ni Bakari
Mbonea, mkazi wa Handeni wakati waliopo kituo cha afya Mkata ni Joseph Mafita
(46), mkazi wa Dar es Salaam, Bilhud Hamisi (61), mkazi wa Moshi, Moris Daniel
(34), mkazi wa Dar es Salaam na mtoto wa miezi minane, Giftclisantus Temba,
ambaye hata hivyo amekabidhiwa kwa baba yake kwa uangalizi zaidi.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment