MAWAKILI wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima, wameandika barua kuliomba Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, kuandika kimaandishi nyaraka wanazozihitaji azipeleke pamoja na vifungu
vya sheria vinavyomtaka awasilishe nyaraka hizo.
Barua hiyo iliyosainiwa na Wakili Peter Kibatala
iliwasilishwa jana mchana katika jeshi hilo, ikiwa ni siku moja baada ya jeshi
hilo kumtaka Askofu Gwajima kuwasilisha nyaraka 10, Aprili 16 mwaka huu
watakapoendelea na mahojiano.
Gwajima aliitwa kuhojiwa na jeshi hilo mara
mbili kutokana na kufunguliwa jalada la malalamiko ya kumkashifu Askofu Mkuu wa
Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo.
Katika barua hiyo, mawakili hao kwa niaba ya
mteja wao wanaliomba jeshi la polisi kumwandikia barua rasmi kimaandishi,
Gwajima wakiainisha nyaraka wanazozihitaji pamoja na vifungu vya sheria
vinavyotumikana jeshi hilo kutaka nyaraka hizo.
Mawakili hao wanasema watashukuru kupata hati
hiyo ambayo hawaijui jina lakini wanaamini jeshi la polisi litafahamu jina la
kisheria la nyaraka husika inayotumika kumtaka Gwajima awasilishe nyaraka
wanazozihitaji.
Aidha wanasema Askofu Gwajima atakapopata
nyaraka anayoihitaji atatimiza wito na kuchukua hatua stahiki za kisheria.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment