Friday, April 17, 2015

Ajali yatokea Rungwe Mbeya ambapo gari aina ya Hiace imetumbikuia mto Kiwira na watu zaidi ya 20 wanahofiwa kupoteza maisha





Taarifa iliyotufikia hivi punde toka Wilayani Rungwe, Jijini Mbeya inaeleza kuwa Basi dogo aina ya Toyota Hiace imetumbukia kwenye Mto Kiwira mapema leo na inadaiwa kuwa zaidi ya watu 20 waliokuwepo kwenye basi hilo wamepoteza Maisha.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, amesema kwamba ajali hii imetokea wakati Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mbeya na Kyela (maarufu kama Coaster) kugoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo hayo, hivyo baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria, hali iliyopelekea hiace hizo kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wake.

Inaelezwa kuwa gari hiyo ilipoteza muelekea na kuingia mtoni, baada ya dereva wake kushindwa maarifa kutokana na mwendo aliokuwa nao.

Mungu aziweke pema roho za marehemu hao,Amin.
MICHUZI

No comments:

Post a Comment