Mwanamke mmoja, mkazi wa Mabibo Mwisho, jijini Dar es
Salaam, anadaiwa kuanzisha danguro la wasichana na kuendesha biashara ya ngono
ikiwamo ya jinsia moja.
Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la mama Uzuri,
anadaiwa kuwachukua wasichana
hao kutoka vijijini kwa kuwadanganya kuwa
anakwenda kuwatafutia kazi mjini.
Inadaiwa kuwa fedha anazopata kutokana na biashara hiyo,
huzitumia kama gharama ya kuwatunza wasichana hao.
Wakizungumza na NIPASHE Jumapili kwa nyakati tofauti,
wasichana hao (majina yanahifadhiwa), walidai kuwa mwanamke huyo aliwachukua
vijijini kwao kwa ahadi ya ajira za ndani.
Wakielezea undani wa biashara hiyo, walisema wanaume
wengi wamekuwa wakiwalazimisha kufanya mapenzi bila kinga (kondom), kwa madai
kuwa kwa kufanya hivyo kunawanyima starehe ya tendo hilo.
Suzana (sio jina lake halisi), alisema makazi yao ni
nyumbani kwa mwanamke huyo ambapo hulelewa katika mazingira mazuri, na kati yao
kuna makahaba na wasagaji.
Alisema, mwanzo walipoanza biashara hiyo walipata wakati
mgumu lakini kadiri siku zinavyokwenda waliizoea.
Alisema baadhi yao wanachukuliwa na wanaume zaidi ya
mmoja kwa siku na wakati mwingine
hugeuka kuwa walimu kwa wasichana wapya wanaoletwa kutoka vijijini.
“Wakati nachukuliwa kwa wazazi wangu, mwajiri wangu
aliwaeleza kwamba nakuja kufanya kazi za ndani kwa ndugu yake, na kamwe
sitopata madhara yoyote kutokana na ulinzi na usimamizi nitakaoandaliwa, lakini
baada ya kufika hali ikawa tofauti," alisema na kuongeza:
“Nilipokelewa vizuri na wasichana wenzangu niliowakuta,
lakini nilishangazwa na kauli ya mwajiri wangu kuwa nahitaji kufanyiwa
ukarabati wa kutosha, na akatoa agizo kutofanyishwa kazi yoyote badala yake
nipumzike na nitaandaliwa kila kitu ninachokitaka, lakini atakaponituma sehemu
na wenzangu nikatekeleze kama atakavyoniagiza, alisema Suzana.
Uchunguzi wa NIPASHE katika mahojiano na mwanamke huyo,
alisema ni vigumu kuiacha biashara hiyo kwa sababu aliianzisha siku nyingi
akiwa na wasichana watano.
Alisema wasichana hao amewaajiri kwa gharama kutokana na
shughuli wanazozifanya, na wanapokwenda
kijijini kwa wazazi wao, huwagharamia matumizi na zawadi kwa familia zao.
Alisema gharama za biashara hiyo hutofautiana kulingana
na kiwango cha mteja, lakini kwa wale wanaofanyiwa tendo hilo kinyume na
maumbile, wateja hutozwa Sh. 20,000, na ngono ya kawaida Sh. 5,000 hadi Sh.10,000 kwa mara moja.
Aidha, alisema wanaofanya tendo hilo kwa jinsia moja
(wasagaji), gharama zake hazitofautiani.
“Kifupi wasichana
wangu wanajituma hata wateja wenyewe wanawakubali ndani na nje ya Dar es
Salaam, lakini biashara ina msimu, kuna wakati inakulipa na wakati mwingine
inasuasua.
“Kikubwa ni ujanja na namna ya kuwaandaa wasichana, kwa
bahati nzuri katika familia zao hakuna anayejua kazi anayoifanya mtoto wake
zaidi ya ‘house girl’. Ni marufuku kutoa siri ya kazi hivyo ni lazima niwekeze
kwao kwa gharama yoyote maana najua wanachokifanya mjini,” alijitapa mwanamke
huyo.
Alisema ingawa anajua kuna maradhi lakini amekuwa mstari
wa mbele kutoa elimu kwao ili waweze kujikinga na magonjwa hatari yanayoenezwa
kwa njia ya ngono pamoja na ugonjwa hatari wa Ukimwi.
No comments:
Post a Comment